Tunamshukuru Mungu kwa kutupa uzima kuadhimisha Sherehe ya watoto na vijana katika Vituo vyetu 11 vya maendeleo ya huduma ya mtoto na kijana . Sherehe hizi ni kumbukizi ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambayo hujulikana kama Krismass. Sherehe hizi zilihudhuliwa na Uongozi wa kanisa, mama wa upendo, wazazi, CYTs, kamati, Watendakazi waalikwa mbalimbali pamoja na viongozi toka Serikarini, tunamshukuru Mungu. Watoto wakifurahia Mchezo wa Viti Ibada iliendeshwa na watumishi wa Mungu Mchungaji Peter Msengi Akifurahi Pamoja na Watoto Vijana walionesha namna walivyoiva kwa utengenezaji wa viatu. Vijana hawa wana kikundi cha Skauti kilichosajiliwa na wanafanya kazi vizuri, kwa sasa wanaendelea na utengenezaji wa viatu na kuuza na pesa kuingia katika akaunti na kuendeleza mradai wao. Kwa sasa wanauwezo wa kupima na kutengeneza kiatu cha aina yeyote kutegemea na hitaji la mteja. Walengwa baadhi walipokea zawadi za mwaka kwa matukio mbalimbali amabayo wameones...