Skip to main content

Maadhimisho ya Sherehe ya Chrismass Kwa Vijana na Watoto

 Tunamshukuru Mungu kwa kutupa uzima kuadhimisha Sherehe ya watoto na vijana katika Vituo vyetu 11 vya  maendeleo ya huduma ya mtoto na kijana . Sherehe hizi ni kumbukizi ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambayo hujulikana kama Krismass.  Sherehe hizi zilihudhuliwa na Uongozi wa kanisa, mama wa upendo, wazazi, CYTs, kamati, Watendakazi waalikwa mbalimbali  pamoja na viongozi toka Serikarini, tunamshukuru Mungu.




Watoto wakifurahia Mchezo wa Viti

Ibada iliendeshwa na watumishi wa Mungu

Mchungaji Peter Msengi Akifurahi Pamoja na Watoto

Vijana walionesha namna walivyoiva kwa utengenezaji wa viatu. Vijana hawa wana kikundi cha Skauti kilichosajiliwa na wanafanya kazi vizuri, kwa sasa wanaendelea na utengenezaji wa viatu na kuuza na pesa kuingia katika akaunti na kuendeleza mradai wao. Kwa sasa wanauwezo wa kupima na kutengeneza kiatu cha aina yeyote kutegemea na hitaji la mteja. 

Walengwa baadhi walipokea zawadi za mwaka kwa matukio mbalimbali amabayo wameonesha katika kipindi cha mwaka mmoja. (Kitaaluma, Usafi, Kujituma kazi, Ujuzi binafisi, uwezo katika masomo ya mitaala pamoja na nidhamu na heshima)


Vijana Mbalimbali walitoa shuhuda zao, zilizogusa maisha yao na kulishukuru Kanisa kwa kutimiza ndoto zao amabazo wanaziona kutimia tulikuwa na Aron John anayesomea Lab ngazi ya Dip, Oscar Shaltiel anayesomea Teaching Dip, Naomi John anayesomea Medical Officer Dip, Kulwa Salumu nayesomea RECORD Mang na mtoto Junur Kanola huyu alishuhudia namna zawadi iliyopokea ilivyobadirisha maisha yake.  Haya yote yalisisimua na kuleta hamasa kwa vijana wengine kufuata nyayo za vijana hawa na mtoto huyu



Mwisho: 

Sherehe yetu iliisha kwa kushiriki chakula cha pamoja, vijana, watoto na wageni wote.



Comments